watu wengi husumbuliwa na tatizo la ngozi zao kuzeeka haraka, kukosa mvuto na kupoteza mvuto wake wa asili, wengi husumbuliwa na mapele, chunusi, ngozi kukauka, madoa na mashimo kwenye ngozi, na hii husababisha wengine kutumia gharama kubwa kununua vipodozi kwa ajili ya kutibu ngozi zao. leo nitawaletea dondoo chache tu za kufanya na kutunza ngozi yako ili iendelee kuwa na mvuto.
1. Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako
watu wengi huharibu ngozi yao wenyewe bila kujua kutokana na kutumia vipodozi visivyoendana na ngozi zao, utakuta mtu ana ngozi yenye mafuta lakini anatumia vipodozi vya watu wenye ngozi kavu, au mtu mwenye ngozi kavu anatumia vipodozi vya mtu mwenye ngozi ya mafuta, hapo lazima ngozi yake itaharibika.
Post a Comment