.Jinsi ya kujua kama unene wako
umepitiliza
Kuna kanuni
iitwayo BODY MASS INDEX (BDM) ambayo humuwesha mtu kujua kama uzito wake
umezidi na maisha yake yapo hatarini.
Kwa kawaida uzito wa mwili hutegemeana na kimo cha mtu,
umri na jinsia. Kanuni hii (BMI) hutupatia uwiano wa uzito wa
mwili wa mtu pamoja na urefu wake.
BMI = Uzito wa mwili katika
kilogramu (Kg) / Urefu wa mwili katika mita za mraba (M^2).
Kutokana na kanuni hiyo,
ukichukua uzito wa mwili wako katika vipimo vya kilogramu, ukagawanya na urefu
wa mwili wako katika vipimo wa mita, utapata namba ambayo kitaalamu
itakuwezesha kujua kama uzito wa mwili wako upo sawa kwa maana ya kama ni uzito
mkubwa au mdogo.
Mfano; mimi nina urefu wa Mita 1.75 na nina uzito wa kilogram
70kg.
Hivyo itakuwa hivi;
BMI= uzito (Kg) ÷ Urefu² (m2)
BMI = 70Kg ÷ (1.75m×1.75m)
= 70kg÷ 3.0625m²= 22.86kg/m² (uzito unaofaa)
BMI huwa na viwango mbalimbali vilivyowekwa na shirika la Afya duniani
(WHO) kutafsiri hali ya lishe ya mtu ambavyo ni;
· BMI chini
ya 18.5 = uzito pungufu.(under weight)
· BMI kati
ya 18.5- 24.9= uzito unaofaa.(Normal weight)
· BMI kati
ya 25.0- 29.9 = unene uliozidi.( over weight)
· BMI ya 30
au zaidi = unene uliokithiri (Obesity)
![]() |
KITABU CHA 3 ZA KUPUNGUA UNENE HARAKA KINAUNZWA ONLINE WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0717254447 WHATSAPP 0788709100 |
uzito wa
mwili hutofautiana kutokana na umri na jinsia ya mtu, mfano uzito wa mwanamke
na mwanaume hutofautiana, pia uzito wa kijana mwenye miaka 18 na mwanaume wa
miaka 40 hutofautiana, hivyo hivyo mtu mrefu huwa na uzito mkubwa kuliko mtu
mfupi.
Zingatia:
- kanuni ya
BODY MASS INDEX (BDM) haitumiki kwa watu wenye ulemavu wa viungo kama viwete,
vilema na watu wasiokuwa na baadhi ya viungo vya mwili kama mikono na miguu
-watoto
chini ya maika kumi na nane wana kipimo chao maalumu cha BODY MASS INDEX (BDM)
-kanuni hii
ya BODY MASS INDEX (BDM) haitumiki wa wanawake waliotoka kujifungua ndabi ya
miezi 6
-vilevile
kanuni hii ya BODY MASS INDEX (BDM), haitumiki kwa wanawake wajawazito,
wanawake wajawazito wana viwango vyao maalumu vya kujua ujito wao kama uko sawa
umezidi.
Watu wengi
huwa hawazingatii kanuni hii, na wengine hata hawaijui, hivyo basi ni muhimu
kuijua kanuni hii na kuitumia mara kwa mara ili kuweza kujua kama uzito wa mwii
wako uko sahihi. Anza leo na utapata matokeo mazuri hapo baadae.
KITABU CHA 3 ZA KUPUNGUA UNENE HARAKA KINAUNZWA ONLINE WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0717254447 WHATSAPP 0788709100
Post a Comment