1.kata ncha za nywele zako
2.onya nywele zako angalau mara moja kwa wiki
3.tumia shampoo inayoendana na nywele zako
tumia shampoo inayoendana na nywele zako, kuna nywele za aina tofauti. kuna nywele kavu, zenye mafuta, mchanganyiko, na pia kuna nywele nyepesi, laini, ngumu na nzito. zipo aina tofauti za shampoo zinazoendana na aina ya nywele zilizopo . hivyo basi ni vyema unapotaka kuosha nywele ukajua ni aina gani ya shampoo utumie, pia kwenye condition napo unatakiwa kufanya hivyo hivyo.
4.Zipe nywele nafasi
nywele nazo huitaji nafasi,kuchana nywele kila siku, kuzipaka nywele jelly kila siku, kuzichana mitindo tofauti, kuziwekea gundi na mafuta tofauti tofauti huzifanya nywele zako zichoke na kukosa afya. hivyo unatakiwa mara moja moja unazipa nywele zako nafasi ya kumupumzika. zipumzishe nywele zako kwa kusuka mtindo ya kawaida au rasta za mabutu.
5.usichane nywele kwa nguvu zikiwa mbichi.
jaribu kuzichana nywele kwa kichanuo kikubwa, au jaribu kuziacha mpaka zikauke ndo uzichane. unapochana nywele mbichi tumia kitana kikubwa na chana taratibub ukianzia nyuma kuja mbele. kuchan nywele zikiwa mbichi bila kufuata utaratibu kutafanya nywele zako zikatike na ziharibike.
6.zilinde nywele zako unapokuwa unaogelea
unapokuwa unaogelea baharini au kwenye bwawa la kuogelea, jaribu kuzifunika nywele zako au zipake mafuta ya kuzui zisiharibike na maji, na unapotoka kuogelea zisafishe nywele zako kwa maji safi na uzikaushe.
7.kula vyakula venye protin na matunda
kula vyakula venye protin na matunda kutasaidia kuimalisha afya ya nywele zako na kuzifanya ziwe nzuri na za kuvutia.
8.Zifunge nywele zako kabla ya kulala
unapotaka kulala hakikisha unazifunga nywele zako, unaweza kuzisuka mabutu au kuzifuna vizuri na kuzibana. kulala huki ukiwa umeziachia nywele zako hufanya nywele zikatike na kuharibika
9.Tumia mafuta asili
badala ya kutumia mafuta yenye kemikali nyingi kutoka viwandani, jaribu kutumia mafuta ya asili katika kutunza nywele zako. tumia mafuta kama ya nazi au parachichi kupaka nywele zako.
10.zilinde nywele zako na jua
wakati utakapokuwa unaelekea kwenye sehemu yenye jua kali, vumbi au upepo. zilinde nywele zako kwa kuzifunika na kofia, scarf au mtandio. pia unaweza kuzipaka sunscreen.
Ncha za nywele unajuaje
ReplyDeleteMzuri sn
ReplyDeleteAhsante sana kwa somo zuri
ReplyDelete