1.Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako
watu wengi huharibu ngozi
yao wenyewe bila kujua kutokana na kutumia vipodozi visivyoendana na ngozi zao,
utakuta mtu ana ngozi yenye mafuta lakini anatumia vipodozi vya watu wenye
ngozi kavu, au mtu mwenye ngozi kavu anatumia vipodozi vya mtu mwenye ngozi ya
mafuta, hapo lazima ngozi yake itaharibika.
2.usilale na makeup usoni
unapokuwa umetoka nyumbani na kurudi usiku usilale na makeup usoni, hata mchana unapoamua kulala usilale na makeup, unapolala mwili huitaji kupumzika na ngozi huitaji kupumua, makeup huziba matundu ya ngozi hivyo kuzui ngozi kupumua vizuri na matokeo yake husababisha ngozi kuchoka, kuzeeka haraka na wakati mwingine kupata mapele au machunusi, hivyo kabla hujalala hakikisha umeondoa makeup zote kwa kutumia makeup remover.
3. safisha uso kabla ya kulala
kama hautaoga usiku au kabla ya kulala basi hakikisha umesafisha uso wako kwa maji safi na sabuni kabla ya kulala hata kama haukupaka vipodozi usoni, ngozi ya uso ni ngozi ambayo hukumbana na changamoto nyingi, hivyo ni vema ukahakikisha umesafisha ngozi ya uso kabla ya kulala ili kuipa ngozi nafasi ya kupumua vizuri
4.kunywa maji mengi
Ili kufanya ngozi yako iwe na mvuto kunywa maji mengi, angalau lita moja na nusu kwa siku, maji pamoja na kusafisha mwili huongeza unyevu kwenye ngozi, kinga na kuondoa sumu kwenye ngozi
5.usitumie vipodozi venye kemikali mbaya
usitumia vipodozi vyenye kemikali kali zisizofaa kutumiwa na binadamu, kemikali kama mercury au hydrochloric asidi ni hatari sana kwa afya ya ngozi na mwili wako kwa ujumla. kemikali hizi ambazo ukianza kutumia hukufanya uonekane mweupe na mwenye ngozi ya kuvutia baada ya mda hubadilika na kuharibu ngozi yako pamoja na kukuletea matatizo ya kiafya
6.kula chakula bora
kula vyakula bora venye vitamini na proteni, kama matunda mboga za majani na vyakula vevye proten kama samaki, mayai, maharage na kuku.
7.jikinge na jua
unapokuwa juani funika ngozi yako kwa mwamvuli au nguo, pia uanaweza kujipaka mafuta maalum kwa ajili ya kujikinga na jua. miale ya jua huunguza ngozi, huondoa mafuta ya kwenye ngozi, hufanya ngozi kuwa nyeusi na huweza kusababisha kansa. jua baya kwa ngozi ni lile la mchana, jua linalofaa kwa ngozi ni lile la asubui na jioni
8.paka mafuta na vipodozi vinavyoendana na hali ya hewa
hali ya hewa hubadilika, kuna majira ya kiangazi ambayo hukausha ngozi, kipupwe ambapo huwa na baridi na upepo na majira ya joto na mvua ambayo huwa na unyevu mwingi, hali ya hewa husabaisha ngozi nayo kubadilika. hivyo ila kuafanya ngozi yako isiathiriwe na hali ya hewa unatakiwa kubadilisha vipodozi kuendana na hali ya hewa
Post a Comment